WEMA AJIVUNIA KUTUA MZIGO WA MWILI

Wema Sepetu

DIVA wa sinema za Kibongo, mwenye nyota ya kipee Wema Sepetu amesema mwili aliokuwa nao huko nyuma ulikuwa ni sawa na mzigo kwake lakini kwa sasa anajiona mwepesi baada ya kuupunguza.  Wema ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa maoni tofauti ya wadau wake kuhusiana na mwonekano wake wa sasa ambao kwa maelezo yake mwenyewe, anasema amepungua kilo 20, jambo ambalo hakutegemea maishani mwake.

“Kwa kweli najisikia mwepesi sana, naweza kufanya chochote kwa sasa hata kama ukinikimbiza sasa hivi huwezi kunipata, kitu ambacho nilikuwa siwezi kufanya huko nyuma. Kwa kweli naufurahia sana mwili wangu,” alisema Wema

 

STORI: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment