WEMA ALA SHAVU ZANZIBAR

Wema Sepetu

LICHA ya kusemekana kwa sasa ustaa wake umepungua, staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu amekula shavu baada ya kualikwa kama mgeni rasmi kwenye Usiku wa Zanzibar Sweetheart utakaofanyika Zanzibar Beach Resort hivi karibuni.  

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wema alisema tayari ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni saba hivyo anamshukuru muandaaji wa tamasha hilo kwa kuona umuhimu wake na kwamba ametambua bado anapendwa.

“Bado nina mashabiki wengi sana maana mpaka nimeweza kupata nafasi hii siyo mchezo, ninawashukuru sana waandaaji kunipa nafasi hiyo na hapo kila mmoja ataona muonekano wangu siku hiyo ya tarehe moja mwezi ujao,” alisema Wema.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Toa comment