Wema ampigia saluti Diamond

wema (2)Wema Sepetu ‘Madam’

Stori: Imelda Mtema

MTOTO mzuri Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ ameonesha kumpigia saluti mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuguswa na ubora wa wimbo wake mpya uitwao Utanipenda kwa kuposti video mtandaoni ikimuonesha akiuimba wimbo huo.

DIAMOND (4)Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Kwenye video hiyo, Madam anaonekana akiwa na shosti wake mwigizaji Aunt Ezekiel wakiimba wimbo huo kwa staili ya kupokezana huku wakiwa wamejilaza kitandani.

Mmoja wa marafiki wa Madam aliyeiona video hiyo, alisema zilipendwa huyo wa Diamond amejirekodi video hiyo kwani ameukubali na unagusa hisia za kila mtu ndiyo maana akajikuta amejirekodi na kuutupia katika Mtandao wa Instagram bila kujali kwamba walishamwagana.

Alipotafutwa Madam kuhusiana na ishu hiyo, alisema amejirekodi video hiyo kwani ameikubali na amekuwa akipenda sana nyimbo za Diamond hata kabla hawajawa na uhusiano na isitafsiriwe kwamba anataka kurejesha majeshi.

“Nilipenda nyimbo zake hata kabla hatujawa kwenye uhusiano na mimi nitaendelea kuwa shabiki wa nyimbo zake siku zote, mapenzi yalishakufa,” alisema Madam.


Loading...

Toa comment