Wema amtoa chozi Diana

MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye kwa sasa amejichimbia nchini Marekani, Diana Kimari amejikuta akimwaga chozi baada ya kumkumbuka shoga’ke kipenzi, Wema Isaac Sepetu.

Diana ameiambia OVER ZE WEEKEND kwa njia ya simu kutoka kwa Trump kuwa, Wema alikuwa mtu wake wa karibu, lakini anahisi ukaribu wao unatoweka kila kukicha baada ya kuanzisha maisha mapya huko aliko ambako hana mpango wa kurejea Bongo.

“Huku Marekani kila mtu ni mpya kwangu, nawakumbuka mno watu wangu wa nyumbani, nimejikuta ninamkumbuka Wema hadi nalia,” anasema Diana ambaye aliondoka Bongo tangu mwaka jana.

STORI: IMELDA MTEMA


Loading...

Toa comment