The House of Favourite Newspapers

WEMA AMTOSA RASMI BWANA’KE

KIMENUKA! Ule uhusiano wa kimapenzi ulioibuka kwa mbwembwe kati ya staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Lawrence Masanja ‘R.A.H.U.R’ unadaiwa kufikia mwisho baada ya Wema kuamua kumwaga manyanga.  Chanzo chetu cha kuaminika kilicho karibu na staa huyo kilimtonya mwandishi wetu kuwa, kuvunjika kwa penzi hilo kulitokana na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Wema kumng’ata sikio kuwa jamaa aliyenaye hafai na akiendelea naye atakuja kujuta.

“Wema kaamua kumwaga manyanga kwa yule jamaa yake, mwenyewe alishaanza kushitukia kuwa kaingia ‘cha kike’ na hata watu wake walipomtonya kuwa jamaa siyo hakuona ugumu kumtosa. Sasa hivi nasikia ana jamaa mwingine,” alidai mtoa habari huyo.

Kufuatia ubuyu huo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kufika nyumbani kwa Wema maeneo ya Mbezi- Salasala jijini Dar ambapo taarifa zilizopatikana hapo ni kwamba, jamaa huyo siku hizi amekata mguu kwenda baada ya kuzinguana na staa huyo. “Law ana muda kidogo hajafika hapa, ninachojua ni kwamba Wema hayuko naye ila siwezi kuongea zaidi kwa kuwa hayanihusu,” alisema kijana mmoja aliyekutwa nyumbani hapo.

Wema huyu hapa Kufuatia kumwagika kwa ubuyu huo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopatikana alisema kuwa hayuko na mshkaji huyo. “Jamani huyo mtu siko naye na sidhani kama itakuwa ni vyema nikimuongelea kwa sababu sihitaji kufanya hivyo ila kwa kifupi hayupo katika maisha yangu,” alisema Wema.

Lawrence alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea kabisa japokuwa alipigiwa mara nyingi na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu. Walifikia pazuri Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao walishafikia pazuri kwani ilidaiwa walikuwa na mpango wa kuingia kwenye uchumba rasmi kabla ya kujihalalisha kwa kufunga ndoa. Tetesi hizo za Wema kutaka kuolewa na Law ziliwahi kumfikia mama Wema, Miriam Sepetu ambaye alionesha kuwaka na kusema hamtambui mwanaume huyo na wala hakuna suala la mwanaye kuolewa.

“Mimi sitambui kabisa kama kuna mchumba eti anataka kumuoa Wema,” alisema Mama Wema alipoongea na mwandishi wetu hivi karibuni. Wema amekuwa akiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti kisha kumwagana nao licha ya kwamba ndoto yake ya muda mrefu ni kuzaa na ikibidi kuolewa kabisa

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Comments are closed.