The House of Favourite Newspapers

Wema amwaga chozi kaburini kwa Mwl. Nyerere

0

Wema Isaac Sepetu akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tunakukumbuka Mwalimu! Beautiful Onyinye kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kupitia Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao, amejikuta akimwaga chozi kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita baada ya mrembo huyo na mastaa wenzake walipotembelea kaburi hilo lililoko kijijini kwake, Butiama Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Wasanii wakiwa katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu kwenye msafara huo, Wema na wenzake waliamua kuzuru kaburi hilo kwa ajili ya kutoa heshima na kumuenzi mwasisi huyo wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao imelenga kuzunguka mikoa mbalimbali nchini kuwahamasisha akina mama ili wawashawishi vijana wao kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Baadhi ya mastaa wa Bongo Movies walioongozana na Wema ni pamoja na Salome Urassa ‘Thea’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’, Mayassa Mrisho ‘Maya’ Sabrina Rupia ‘Cathy’ na wengine kibao.

Leave A Reply