Wema ana rekodi yake Miss TZ

MIONGONI mwa warembo waliotwaa Taji la Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu ndiye mwenye rekodi yake ya kipekee ya kuwa na skendo nyingi ambazo zilijulikana na kuandikwa.

Kwa mujibu wa tathmini ya Ijumaa Wikienda, skendo ya kwanza kuhusu mrembo huyo ni ile ya kushiriki shindano hilo akiwa na umri wa chini ya miaka 18, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.

 

Habari ya kwanza kuhusu mrembo huyo kuwa ‘anda 18’ iliandikwa kwa mara ya kwanza na Ijumaa Wikienda, mwaka 2006 wakati Wema alipokuwa Warsaw nchini Poland ambako Fainali za Miss World zilichukua nafasi.

Mara baada ya kurudi nchini akitokea Poland ambako alifanya vibaya, Wema alianza kuandamwa na skendo mbalimbali za kukamatwa na kulala mahabusu kisha za ngono, rekodi hii hakuna mwingine mwenye nayo.

 

Katika kipindi chote cha ustaa wake yapata miaka 12, Wema alihusishwa kutoka kimapenzi na watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasiasa, mastaa wa Bongo Fleva, Khaleed Mohammed ’TID’, Herry Samir ‘Mr Blue’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, waigizaji akiwemo marehemu Steven Kanumba, wajasiriamali akiwemo Jumbe Yusuf Jumbe na wengineo kama Mshindi wa BBA, Idris Sultan, Clement, Nagari Kombo, Luis Mnana na Patrick Christopher ‘PCK’.

STORI: SIFAEL PAUL

List yaMastaa Wa Bongo Wanaoishi Kwenye Nyumba Za Ghorofa

Toa comment