Wema Atamba Mungu Kumtendea Miujiza Atarajia Kufanya Pati Kubwa
WEMA Isaac Sepetu; ni staa ambaye nyota yake kushuka ni shida Bongo, anasema kuwa watu wamuachie uwanja kwa maana mwezi huu wa Septemba ni mwezi wake wa kuzaliwa hivyo anahitaji kupendeza kila kukicha mpaka siku yake ifike ndiyo maana anaweka mambo matamumatamu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Wema ambaye ni mhamasishaji wa chanzo ya UVIKO-19 anasema kuwa, anaufurahia mno mwezi huu kwa sababu baadhi ya vitu vyake vinakwenda sawa kama anavyotaka na alivyopanga, kiufupi anasema Mungu amemtendea miujiza.
“Jamani mniache tu, huu ni mwezi wangu jamani, Mungu amenitendea mambo mengi mwaka huu, ni mwaka wangu huu hivyo waniache tu niinjoi mimi,” anasema Wema ambaye anatarajia kufanya pati kubwa ya kumbuziki ya kuzaliwa ifikapo Septemba 28, mwezi huu ambapo atakuwa anatimiza umri wa miaka 31.