WEMA  ATOBOA SIRI YA KUBADILIKA

Wema Isaac Sepetu

STAA ‘grade one’ kunako filamu za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ametoboa siri ya kubadilika kwake kimuonekano kuwa ni kwa sababu amepitia vipindi vigumu. Akizungumza na Za Motomoto, Wema alisema kuwa kwenye maisha lazima mwanadamu apitie vipindi vingi sana vigumu na kipindi cha mwisho ndio unakuta ni chake cha kudumu kama alivyo yeye hivi sasa.

“Najua watu wengi sana sana wanashangazwa na mabadiliko yangu lakini ndio hivyo maana itakuwa ni sehemu ya kudumu ya maisha yangu mengine baada ya kupitia kipindi kigumu,” alisema Wema. Mwaka jana, Wema alifungiwa na bodi ya filamu kujihusisha na kuigiza baada ya kusambaa kwa video na picha zake mitandaoni zilizokosa maadili. Hata hivyo kwa sasa amefunguliwa.

Toa comment