Wema Azua Hofu Ukumbini!

STAA mkubwa kunako filamu za Kibongo ambaye umaarufu wake ulianza baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, amezua hofu ukumbini kiasi cha watu kujiuliza kama ni yeye kweli, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda mzima.

 

Wema alizua hofu hiyo katika uzinduzi wa baa mpya ya mwigizaji na shosti wake, Aunt Ezekiel inayojulikana kwa jina la The Luxe iliyopo Mikocheni jijini Dar.

Wema alizua minong’ono baada ya kuingia ukumbini na wageni waalikwa kuanza kumshangaa jinsi mwili wake ulivyopukutika.

 

Wakati waalikwa wakiendelea kupata kilaji kwenye baa hiyo yenye muonekano wa kisasa, walianza kuingia mastaa mbalimbali ambao hawakuwashtua, lakini taharuki ilizuka baada ya Wema kuibuka ghafla.

Wanaomfahamu kwa ukaribu waliokuwepo ukumbini hapo walimvaa na kukumbatiana naye huku wakionesha kumshangaa alivyo.

 

Minong’ono ya aina yake ilianza kutawala kila kona wengi wakizungumzia jinsi mwili wake ulivyopungua na kumfanya akongoroke mpaka usoni.

“Yaani huyu ni Wema kweli au mtu mwingine maana siyo kwa kupukutika huku, jamani kama anatumia dawa za kujipunguza ni bora akaachana nazo tu maana anageuka kituko sasa.

 

“Alipoingia na mapaparazi kumkimbilia sikujua kama ni yeye nilidhani ni mtu mwingine baada ya muda ndipo akagundua kumbe alikuwa ni Wema, jambo lililonishangaza kutokana na umbo lake alivyopungua, jinsi alivyopungua,” alisikika mrembo mmoja akizungumza na mashosti zake.

 

Mwanahabari wetu alifanya jitihada za kutaka kuzungumza na Wema, lakini baada tu ya salamu wapambe aliokaa nao walimzuia kufanya mahojiano.

“Yaah tutaongea, nitafute wakati mwingine hapa si unaona mambo yalivyo mengi,” alisema Wema ambaye hata hivyo, alipotafutwa siku iliyofuata simu yake haikupatikana hewani.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR


Loading...

Toa comment