Wema: Dhambi Hii Imeniepuka

SUPASTAA mwenye jina lake kunako Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu anafunguka kuwa, kama kuna dhambi ya kuchora tatuu ya jina la mwanaume mwilini, basi kwa upande wake imemuepuka.
Wema anasema kuwa, hii ni kwa sababu hakuna mwanaume wa kumuamini duniani zaidi ya baba mzazi ambapo yeye amemchora baba yake mzazi, marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.
Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA juzikati, Wema anasema kuwa, hakuna kitu ambacho mwanaume anaweza kumfanyia kiasi kwamba akajikuta anamchora jina mwilini mwake, zaidi ya wazazi au watoto wake siku atakapobarikiwa kuwa nao na siyo wengine.
“Yaani mwanaume ambaye nimempa nafasi ya kumchora kwenye mwili wangu ni baba yangu peke yake na si mtu mwingine maana sijaona maajabu aliyofanya mwanaume kwangu mpaka niende kabisa kumchora tatuu.
“Hata kama atatokea mwanaume akafanya maajabu, bado hana nafasi ya kumchora kwenye mwili wangu maana hata kwa Mungu nitaulizwa hilo,” anasema Wema ambaye kwa sasa ana mpenzi wake ambaye hataki kumfanyia matangazo kwenye mitandao ya kijamii.
STORI; IMELDA MTEMA, DAR

