Wema, Mbunge wa Chadema, Wapanda Miti Moro
MSANII wa filamu na mlimbwende maarufu nchini, Wema Sepetu, ‘Madam’ ambaye hivi karibuni ameipasua Bongo Muvi kwa kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshirikiana na Mbunge wa Viti Maalum wa Morogoro, Devota Minja na wanawake wengine mjini humo kupanda miti.
Ikiwa leo ni siku ya Wanawake Duniani, Wema ameungana na wanawake wa Mkoa wa Morogoro kuadhimisha siku hii kwa kupanda miti kwa lengo la kupunguza joto na kero ya maji hapo baadaye.
Aidha Wema ameendelea kuwahimiza mashabiki wake wamuite Kamanda, jina alilojibandika baada ya kukabidhiwa kadi ya chama hicho.
Comments are closed.