Wema, Mbunge wa Chadema, Wapanda Miti Moro

Wema na baadhi ya wanachama wa Chadema

MSANII  wa filamu na mlimbwende maarufu nchini, Wema Sepetu, ‘Madam’ ambaye hivi karibuni ameipasua Bongo Muvi kwa kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshirikiana na Mbunge wa Viti Maalum wa Morogoro, Devota Minja na wanawake wengine mjini humo kupanda miti.

Mbunge wa Chadema wa Kwanza (kulia) na Wema na wanachama wengine wa chama hicho

 Ikiwa leo ni siku ya Wanawake Duniani, Wema ameungana na wanawake wa Mkoa wa Morogoro kuadhimisha siku hii kwa kupanda miti kwa lengo la kupunguza joto na kero ya maji hapo baadaye.

Aidha Wema ameendelea kuwahimiza mashabiki wake wamuite Kamanda, jina  alilojibandika  baada ya kukabidhiwa kadi ya chama hicho.

Ujumbe wa Wema mtandaoni

Na Salum Milongo/GPL


Loading...

Toa comment