Wema, Mobeto wamaliza bifu

BAADA ya kuishi kwa muda mrefu huku ikidaiwa hawaivi, warembo Wema Sepetu na Hamisa Mobeto wameonesha kwamba hawana tena kinyongo kati yao baada ya kila mmoja kumfuata mwenzake (kum-follow) kwenye ukurasa wa Instagram.

Kwa nyakati tofauti hivi karibuni, wawili hao walichukua muda wao kufuatana kwenye ukurasa wa Instagram japo haifahamiki ni nani alimuanza mwenzake lakini wananzengo walitupia picha ya wawili hao kuonesha kufuatana na kuwapongeza.

“Kwa hiyo lile bifu kati ya warembo hawa ndio lishaisha? Ila mna akili sana watoto wazuri bora mmemaliza hilo bifu maana mwanaume mwenyewe mnaemgombania kawabwaga wote sa hivi pigeni tuu kazi na msapotiane,” aliandika malkiawaudaku


Loading...

Toa comment