Wema, Mobeto Wapewa Makavu

MASELEBRITI wawili Bongo, Isaac Sepetu na Hamisa Mobeto wapepewa makavu na mshabiki wao baada ya kuoneshana ushosti wa kukomentiana kwenye Instagram.

 

Mobeto ndiye aliyekwenda kwenye ukurasa wa Wema na kuweka maoni katika picha ya mwanadada huyo kwa kumwambia ni mrembo ambapo naye alimjibu kuwa yeye ni mrembo zaidi. Baadhi ya mashabiki walidai kuwa, hawana na hawajawahi kuwa marafiki kwani walishatembea na mwanaume mmoja ambaye ni Mondi.

 

“Hakuna ushosti hapa, wote walishatembea na mwanaume mmoja hivyo kinachotokea hapa ni kila mmoja kwenda pembeni kumsema vibaya mwenzake,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki ya mashabiki hao. Wawili hao hawajawahi kuwa marafiki na Wema alishakariri akisema wazi kuwa hampendi Mobeto.

 

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

 


Toa comment