WEMA: NIKIMSIFIA KIBA KUNA MTU ANATESEKA ?

Wema Sepetu

 STAA wa filamu Bongo Muvi, Wema Sepetu amesema kuwa hawezi kuficha hisia zake kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, kutokana na wimbo wake mpya wa Mbio kuwa mzuri na kuhoji kwani kuna mtu anateseka?

 

Akizu-ngumza na Risasi Mcha-nganyiko, Wema alisema kuwa anapenda kumsifia mtu akiwa anafanya kitu kizuri maana kuficha hisia zako kwa kitu kizuri hiyo inakuwa ni dalili ya roho mbaya ambayo kwa upande wake hataki kuikaribisha roho mbaya kwenye maisha yake ya kila siku.

 

“Ni hivi tuelewane Kiba anaimba bwana huo wimbo wa Mbio ni kiboko, mimi namkubali sana na ni shabiki wake mkubwa siku zote hivyo kama kuna mtu kavimba anune apasuke mimi sijali kabisa,” alisema Wema bila kumtaja jina la mtu anayeteseka.

Toa comment