Wema: Sehemu ya Kuzikwa ni Palepale

KWELI mambo ni mengi muda mchache! Staa wa Bongo Movies asiyechuja, Wema Isaac Sepetu amekumbushia kuwa sehemu atakayozikwa ni palepale pembeni ya baba yake, Balozi Sepetu kule Chuini visiwani Zanzibar.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema amesema ni muhimu kukumbusha watu kila mara maana wanaweza kupitiwa na kumpeleka sehemu ambayo mtu haipendi.

 

“Najua watu wanaweza kujisahau hivyo ni vizuri kuwakumbusha mahali ambapo mtu anataka apumzishwe siku ikiwadia,” amesema Wema.

STORI: IMELDA MTEMA,DAR


Loading...

Toa comment