The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Atangaza Rasmi Kurudi CCM -(Video)

0
Wema Sepetu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

MSANII maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo Ijumaa, Desemba 1, 2017 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa ni kukosa amani ndani ya chama hicho.

Wema ambaye ni alikuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Tanzania 2006, amesema Chadema ni kama nyumba inayomkosesha amani hivyo hana haja ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo.Amesisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM.

Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu walihamia Chadema mwezi Februari mwaka huu baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

ALICHOKIANDIKA WEMA KWENYE AKAUNTI YAKE YA INSTAGRAM

BREAKING: WEMA SEPETU KATHIBITISHA KURUDI CCM! BYE BYE CHADEMA!

 

TUJIKUMBUSHE: Wema Sepetu Arudisha Kadi ya CCM na Kujiunga na CHADEMA (Video)

Leave A Reply