The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu: “Napenda Kuwashukuru Kwa Kuniamini Na Kusimama Na Mimi…”

Wema Sepetu anazidi kuzimiliki headlines za mitandao kinamna yake.

Ukitembelea ukurasa wa Instagram wa staa huyo utakutana na ujumbe mrefu wa shukurani kwa watu wote waliokuwa nae bega kwa bega kwenye kipindi kigumu.

“Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote”. – ameandika Wema Sepetu.

Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu. Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote. Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana. Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu tunasema asanteni sana. #WemaApp hakikisha umedownload kutoka Playstore afu tuongee kule zaidi.. Me and my family would like to take this opportunity to express our sincerely gratitude to all who were with us during the hard time we passed through. I know you were prayed for me, I thank you for your prayers because they helped giving me strength during the time I had a very difficult moment in my life. I would like to thank all of my funs all over the world for trusting and standing with me in all this period, I would like to thank my fellow artists too. Many thanks to my lawyer Advocate Alberto Msando for standing with me and being altogether in this hard time. I pray to God he gives you that heart of defending weak people. Thanks very much. We, the family of the late Abraham Issac Sepetu said thanks to you all You may encounter many defeats, but you must not be defeated. In fact, it may be necessary to encounter the defeats, so you can know who you are, what you can rise from, how you can still come out of it.

A photo posted by A grown Libra (@wemasepetu) on

Wema pia ameendelea kuwakumbusha mashabiki zake wa ndani na nje ya nchi kuendelea kudownload App yake mpya inayopatikana kwa watumiaji wa Android (kwa sasa) kupitia Android Play Store

Kaa karibu na Wema Sepetu kwa kum-follow Instagram (@WemaSepetu), ama bonyeza hapa.

Comments are closed.