The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu: Naumia Sana Nikiona Watoto wa Uwoya, Wolper, Natamani Mtoto

0
Wema Isaac Sepetu

Wema Isaac Sepetu; ni staa ambaye kila kukicha manyota yanazidi kung’aa, lakini bado akiwa na machungu tele moyoni baada ya kutafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio.

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Wema anasema kuwa, hakuna kitu kinachomuumiza kila kukicha kama kuona marafiki zake kama Irene Uwoya, Aunt Ezekiel, Lulu na Jacqueline Wolper wakiwa na watoto wao, lakini yeye bado hajabahatika.

 

Wema anasema kuwa, kuna muda anajisahaulisha kuhusiana na kupata mtoto, lakini baada ya muda kinatokea kitu kinachomkumbusha.

 

“Naanza kuumia sana na ndiyo hali inayonikuta nikiwa na marafiki hao,” anasema Wema ambaye ni mmoja wa memba wa kundi la mastaa hao wanaojiita Big Six na kuongeza;

 

“Yaani mimi naumia sana, natamani sana kusahau hili, lakini ukweli ni kwamba kuna muda natamani na ninapoona rafiki zangu wanawaongelea watoto wao; yaani kama mwanadamu naumia na mimi natamani kubeba mtoto wangu.”

Kwa miaka mingi Wema amekuwa akitoa kilio chake cha kukosa mtoto na amekwishakwenda kwenye matibabu bila mafanikio.

Stori; Imelda Mtema, Dar

WEMA KATIA NENO, PENZI LA DIAMOND NA ZUCHU – “NATAMANI WAOANE, NAMPENDA ZUCHU”

Leave A Reply