The House of Favourite Newspapers

Wema: Sherehe ya Tiffah haikunihusu

0

wemaStaa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘Madam’.

Imelda Mtema

Staa asiyechuja Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa hakuhudhuria kwenye 40 ya mtoto wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alikuwa mpenzi wake kwa kuwa haikuwa inamuhusu.

TIFFAH DIAMOND (3)Staa wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady’ wakimbeba mtoto wao, Latiffah Nasbul ‘Princes Tiffah’.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni baada ya kumuuliza kwa nini hakuonekana kwenye sherehe hiyo, Wema alisema asingeweza kwenda kwa kuwa haikuwa ikimuhusu hata kidogo.

“Sasa jamani ningeenda kwenye hiyo sherehe wakati haikuwa ikinihusu kwa lolote, mfano ningeenda pale kama nani sasa na wala sikuwa najua kama kuna kitu kama hicho kwa sababu sikualikwa,” alisema Wema.

Leave A Reply