WEMA : SIJAZOEA HUU MWILI , NAPEPESUKA

Staa mwenye jina lake Bongo, Wema Abraham Sepetu amesema kuwa hata yeye mwenyewe huo mwili alionao hajauzoea hata kidogo maana kuna wakati anajisikia mwepesi mpaka anapepesuka. Akizungumza na Ijumaa, Wema alisema ni ngumu kuwa na mwili mnene halafu baadaye kuwa mwembamba lazima mabadiliko yatokee hasa ukiwa umeondosha kilo nyingi.

“Kiukweli kuna muda nakuwa bado sijauzoea huu mwili hata kidogo unaweza ukakaa lakini ukiinuka unapepesuka unajua bado una mwili uleule mkubwa,” alisema Wema ambaye ameondoa takribani kilo 25 mwilini mwake.


Loading...

Toa comment