The House of Favourite Newspapers

Wema Siye England Ndiyo Mabingwa Kombe la Dunia

ACHA kabisa kwani mastaa mbalimbali wameonekana kufuatilia kwa ukaribu mkubwa michuano ya Kombe la Dunia, sasa muigazaji Wema Sepetu amesema anaamini timu ya Taifa ya England ndiyo mabingwa wa michuano hiyo mwaka huu.

 

England imeanza vyema michuano ya Kombe la Dunia inayofanyika Urusi baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Tunisia.

 

Wema amejigamba mbele ya mwandishi wa Championi Jumamosi kuwa, England itabeba kombe kwa sababu wachezaji wake wengi ni vijana na wana vipaji vikubwa.

 

“England ndiyo timu yangu nayoishabikia, kama hujui pia ni shabiki mkubwa wa Man United na wachezaji wengi waliopo Urusi wanachezea United kwa hiyo sikuona haja ya kwenda mbali wakati nyota wa klabu yangu wapo England. Matumaini ni makubwa sana ya kutwaa ubingwa kwani hata ukiangalia mchezo wa kwanza tulipata ushindi mzuri wa mabao mawili tofauti na timu nyingine ambazo zinapewa nafasi,” alisema Wema.

Comments are closed.