The House of Favourite Newspapers

Wemi TZ Yagawa Barakoa Bure Kwa Yatima, Bodaboda

0

Taasisi ya Worship Empowerment Ministry Tanzania (WEMI TZ) jana imegawa vifaa vya kuzibia mdomo ‘barakoa’ katika vituo vya watoto yatima vya Umra, Al-Madina na Sifa Group Foundation vilivyoko Vikawe Bagamoyo mkoani Pwani na baadhi ya vituo vya bodaboda.

 

 

WEMI imegawa barakoa hizo ikiwa ni sehemu ya Juhudi ya kuiunga mkono Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Janga hatari la Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Corona.

 

 

Akizungumza kwa niaba ya Mwanzilishi wa WEMI, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili na Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la Revival, Milca Kakete, Mwakilishi wa WEMI Kijiji Dar Es Salaam, Mlapa Ng’osha alisema WEMI imeguswa na namna Serikali ya Rais, Dk John Pombe Magufuli na Wizara ya Afya wanavyopambana na ugonjwa wa Corona ikiwemo kumtanguliza Mungu kama kinga, tiba na mtetezi mkuu, kutoa elimu kwa sekta na makundi mbalimbali.

 

 

“Tumeamua kuiunga mkono serikali yetu ya Rais Dk, Pombe Magufuli kupambana na Janga la korona. Kama WEMI tumegawa Barakoa 200 katika ili kuwasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa KUPATA vifaa hivyo.

 

 

“Barakoa hizo tumegawa katika vituo vya watoto yatima vya Umra, Al-Madina na Sifa Group Foundation vilivyopo, Vikawe, Bagamoyo mkoani Pwani pamoja na vituo kadhaa vya dereva pikipiki (bodaboda).

 

 

“Serikali imejitahidi kwa sehemu yake lakini na sisi kama WEMI tumeguswa na tumeamua kujitoa kuhakikisha Tanzania na Watanzania wenzetu wanabaki salama.

 

 

“Tutaendelea kutoa Elimu stahili kwa kufuata muongozo wa Wizara ya Afya, pia tunampongeza Waziri wake Ummy Mwalimu pamoja na timu nzima kwa Namna inavyopigana,” Alisema Mlapa.

 

 

Taasisi ya WEMI Tanzania yenye makao makuu nchini Canada, imekuwa ikiwawezesha Waimbaji wa nyimbo za Injili na Wachungaji wa Vijijini wanaotoa huduma ya Mungu katika mazingira magumu.

WEMI imekwishagawa baskeli kadhaa kwa baadhi ya wachungaji na kumuwezesha kiuimbaji Mwimbaji Mwenye ulemavu wa macho, Paschali wa Dodoma aliyeimba wimbo wa Nakung’ang’ania remix. Hata hivyo, WEMI wamejipanga pia kutoa barakoa na vitu vingine katika vituo baadhi ya Mkoa wa Dodoma.

 

Leave A Reply