Wentworth Gas Ltd Yasaidia Wasichana wa Shule Za Kitanzania Kwenye Sekta ya Elimu
27 Januari 2023, Mtwara. Kampuni ya Wentworth Gas Ltd, kupitia Taasisi ya Wentworth Africa Foundation Tanzania imetoa taulo 1,500 zenye thamani ya Shilingi milioni 5 kwa watoto wa shule za Mtwara ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo mjini Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali. Ahmed Abbas Ahmed aliishukuru kampuni ya Wentworth Gas Ltd kwa msaada wao katika kuhakikisha wasichana wanabaki shuleni.
Meneja Mkazi wa Kampuni ya Wentworth Gas Ltd, Richard Tainton alisema kuwa kama sehemu ya mpango wa uwajibikaji kwa jamii wa Wentworth, wana programu mbalimbali za kusaidia sekta za Afya, Elimu na Mazingira katika eneo hilo.
‘Nina furaha kuthibitisha kuwa kampuni ya Wentworth Gas kupitia Asasi ya Wentworth Africa Tanzania inaendelea kusaidia jamii ambazo tunafanyakazi kama sehemu ya mpango wetu wa kurudisha kwa jamii. Programu yetu inayoitwa “Keep a Girl in School” unawapa wasichana fursa ya kupata huduma salama na zinazofaa, kama vile vyoo, majisafi, mifumo ya kudhibiti taka na vifaa vya usafi wa hedhi.
Wasichana ambao wanaweza kusimamia usafi wao wa hedhi na kubaki shuleni wana uwezekano mkubwa wa kumaliza elimu yao, ambayo inaweza kuwa na manufaa ya muda mrefu ya kiuchumi. Tunaendelea kushirikisha serikali katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na jamii zenyewe ili kutambua na kuleta athari popote tunapoweza ili kuboresha maisha ya watu ‘- Meneja Mkazi Wentworth Gas Ltd, Richard Tainton.
Kuhusu Wentworth Resources PLC:
Wentworth ni kampuni inayojitegemea iliyoorodheshwa na AIM na mshirika katika Washirika wa pamoja wa Mnazi Bay (pamoja na TPDC, M&P, na CMBL). Kampuni hii inaongoza kwa uzalishaji wa gesi nchini Tanzania. Lengo letu kuu la uzalishaji huko Mnazi Bay, katika mwambao wa bonde la mto Ruvuma, Kusini mwa Tanzania. Kwa historia yetu nzuri na utendaji mzuri wa kifedha, tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu kusaidia Tanzania katika kufikia upatikanaji wa nishati kwa wananchi wote ifikapo 2030.
Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na:
Neema Ndikumwami
Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii
+255 (0) 786 716 318
[email protected]@wentplc.co.tz