The House of Favourite Newspapers
gunners X

Wenye Mimba Ruksa Kurudi Shule

0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari watakaokatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, mimba na changamoto mbalimbali za kifamilia watapewa fursa ya kurejea Shuleni katika mfumo rasmi.

 

Waziri Ndalichako ametoa kauli hii leo akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Sekta ya elimu katika kipindi cha miaka 60 “leo natoa waraka wa elimu ambao utaelezea ni lini Wanafunzi watakaokatisha masomo kwa sababu ya mimba na changamoto nyingine watapaswa kurejea Shuleni, leoleo natoa waraka hakuna kupoa, zege halilali”

Kutokana na umuhimu wa elimu kwa watoto wetu serikali imeamua kuondoa vikwazo vya elimu kwa watoto, wapo baadhi wamepata ujauzito, serikali imeamua wanapokuwa tayari watarudi darasani na watafanya mitihani kama na wakifaulu watapangwa katika shule za serikali”- Prof. Ndalichako.
 
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo leo Novemba 24, 2021 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Sekta ya elimu katika kipindi cha miaka 60.

Leave A Reply