The House of Favourite Newspapers

Weusi: Naliamsha Dude Imeharibu Utaratibu

0
G Nako

MAKALA: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI | SHOW BIZ

TITO Mboweni ni jina maarufu Afrika Kusini. Hutumiwa sana na vijana wa mitaani ambapo mara nyingi linapotajwa na vijana hao basi ujue wanamaanisha pesa.

Hata hivyo, jina hilo halikutungwa tu na vijana hao na kulipa maana. Mboweni alikuwa ni gavana wa nane wa Benki ya Sarb (Sourth African Reserve Bank), aliyekuwa na mafanikio makubwa nchini humo pamoja na historia ndefu.

Mbali na jina hilo kupaishwa na vijana wa mitaani hata baadhi ya wanamuziki wazawa wa taifa hilo akiwemo Cassper Nyovest wamelitumia kwenye ngoma zao kwa maana hiyo iliyozoeleka mtaani.

Nikki wa Pili

Cassper ana wimbo unaoitwa Tito Mboweni.

Hivyo ndivyo sanaa ilivyo.

Kuchukua kitu kinachosikika mtaani ama kuvumbua na kukipaisha zaidi. Na katika hili wasanii hasa wanamuziki wamekuwa wakifanya mara kwa mara.

Tito Mboweni (pesa) likitamba Afrika Kusini, tumeona hivi karibuni kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram mmoja wa wanamuziki wanaounda Kampuni ya Weusi, Nikki wa pili ameposti kipande cha video ikiwaonesha yeye na wanamuziki wenzake, Joh Makini na G Nako wakiimba wimbo uitwao Naliamsha Dude ambao bado hawajaiachia rasmi kwenye media.

Joh Makin

Wimbo huo umeleta kizaazaa mtandaoni na mitaani. Mapokezi yake ni shida! Umeonekana kuwapagawisha kwelikweli watu wengi kiasi kwamba umebadili utaratibu uliokuwepo kwenye kundi hilo.

Pengine unaweza kusema idea ya wimbo huo imepokelewa vizuri kutokana na maneno naliamsha dude kuwa maarufu nchini kwa sasa. Hayo ni maneno ambayo yamepewa kiki na mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na huyatumia zaidi pale anapotaka ‘kuwapiga’ watu waliomchokoza mbele ya ‘familia’ yake pale kanisani kwake Ubungo Maji jijini Dar.

Hilo linawezekana maana akichonga na Uwazi Showbiz, kwa niaba ya Weusi, G Nako amekiri juu ya hilo. Na kusema wao kama Weusi wamekuwa wakitumia mara nyingi majina ama maneno ambayo yanakiki mtaani ili kutengeneza mazingira rafiki ya kazi yao na wapenzi wa kazi zao.

Hata hivyo, mbali na kukiri juu ya hilo G Nako amesema malengo makubwa ya  kuachia kipande cha video wanataka kuachia.

Msikie akifanya mahojiano na Uwazi Showbiz;

Showbiz: Kwa hiyo unataka kusema huo siyo wimbo mpya ambao mlikuwa mnampango wa kuuachia?

G Nako: Ndiyo, kuna kazi nyingine nyingi ambazo zilikuwa kwenye mipango, ikiwemo tuliyofanya na Christian Bella, lakini mapokezi yametufanya tuanze majadiliano ya kuuachia wimbo huo. Naweza kusema ikiwa tutakubaliana kuuachia utakuwa umeharibu utaratibu ambao tulikuwanao awali.

Showbiz: Mmefanyia wapi audio ya wimbo huo?

G Nako: Pale Wanene Entertainment.

Showbiz: Kutokana na mapokezi, video yake mmepanga kuifanyia wapi?

G Nako: Hapahapa Bongo.

Showbiz: Namaanisha na dairekta gani?

G Nako: Tutafanya na madairekta wa hapohapo Wanene Entertainment.

Showbiz: Kipi ambacho hamkukitegemea na mmekiona baada ya kuachia wimbo huo?

G Nako: Ni mapokezi tu kuwa makubwa. Sikufi chi ndani ya muda mfupi watu wameonesha kuelewa sana tulichofanya. Kwa hiyo mambo yakiwa mazuri tunaweza kuiachia ngoma hii.

Showbiz: Kuhusu bajeti ya kurekodia audio mpaka video, inaweza kufi ka shilingi ngapi?

G Nako: Hilo siwezi kulizungumzia zaidi kwa sasa maana kabla ya kurekodi mnaweza kupanga mtumie kiasi fulani lakini mkishaingia ‘location’ baadhi ya vitu vinajitokeza na kuongeza gharama.

Showbiz: Rasmi watu wategemee mtauachia ujio huo lini?

G Nako: Hivi karibuni tu, kama nilivyosema awali bado tupo kwenye mazungumzo na mambo yakiwa kama yanavyoendelea tutauachia wimbo muda si mrefu.

Leave A Reply