The House of Favourite Newspapers
gunners X

WHO Yasitisha Majaribio ya Hydroxychloquine Kama Tiba ya Corona

0

SHIRIKA la Afya ulimwenguni (WHO) limesema linaahirisha majaribio ya dawa ya hydroxychloroquine kama tiba ya ugonjwa wa COVID-19 ambapo mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema wanachunguza usalama wa dawa hiyo.

 

Uamuzi huo wa WHO umefikiwa baada ya ripoti ya wanasayansi iliyochapishwa katika jarida maarufu la kitabibu la The Lancet wiki iliyopita, ikisema matumizi wa hydroxychloroquine yalikuwa yakizidisha hatari ya kufa miongoni mwa wagonjwa wa COVID-19,  amesema Ghebreyesus katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya video jana jioni.

 

Alisema kile kinachofahamika kama ‘mshikamano wa majaribio’ kinachohusisha mamia ya hospitali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikiijaribu dawa hiyo kwa wagonjwa wa virusi vya corona,  kimeacha majaribio hayo kama hatua ya tahadhari. Mkuu wa huduma za dharura wa WHO, Mike Ryan, amesisitiza kuwa hakuna matatizo mengine yaliyojitokeza.

 

Ingawa dawa hiyo awali ilitumiwa kutibu maumivu ya misuli, baadhi ya watu, akiwemo Rais Donald Trump wa Marekani, wamekuwa wakiipigia debe kama tiba kwa virusi vya corona, na nchi kadhaa zimekuwa zikiiagiza kwa wingi.

Wiki iliyopita, Waziri wa Afya wa Brazil alishauri matumizi ya dawa hiyo,  na nyingine ya Chloroquine inayotibu malaria, kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19.

Leave A Reply