The House of Favourite Newspapers

Whozu Aanika Siri Kubwa ya Tunda – Video

0

MSANII wa muziki wa BongoFleva, Whozu amwvunja ukimya na kufunguka namna alivyoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na video vixen maarufu Bongo, Tunda ambapo amedai kuwa bi dada huyo alimpenda Whozu kutopkana na alivyo wala si kitu kingine.

 

Whozu amefunguka hayo leo Januari 6, 2020, wakati akipiga stori kwenye Exclusive Interview ndani ya Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 6:00 mpaka saa 10:00 jioni, kupitia +255 Global Radio.

 

“Mwanamke anaweza kukupenda kwa jinsi unavyo, unavyom-treat, anaweza asikupendee hela zako au kwa ustaa wako, inategemea na namna ambayo ulienda jitambulisha kwake. Mnavyomchukulia Tunda ni tofauti, ni mtu ambaye anaweza kukushauri. Namshukuru ameweza kunipa sapoti kwenye kazi yangu, anapenda kile nachokifanya na anasapoti asilimia mia.

 

“Diamond Platnumz ni moja ya msanii ambaye ana mafanikio makubwa sana na anaitambulisha nchi yetu, mifano yake unaweza kuitumia na wewe ukafanikiwa kama yeye alivyoweza kufanikiwa. Nampongeza amekaa kwenye game miaka 10 sio mchezo, ku-sustain ndio shughuli wengi wanajisahau na kuingia kwenye madawa ya kulevya.

“Muziki unahitaji uwekezaji mkubwa sio kwangu tu hata kwa wasanii wengine pia, hela ya muziki huwa inakuja baadae sana. Muziki ni moja ya biashara ambayo unaweza kutumia nguvu nyingi kuwekeza halafu kwenye ikachukua muda mrefu kurejesha ulich0kiwekeza. Ila namshukuru Mungu kwangu mimi angalau kile niliwekeza kinaanza kurudi.

 

“Ukiwa msanii kuna mawili, unaweza kusemwa kwa mazuri au mabaya pia, hivyo inabidi ukubali vitu vyote unavyoona sababu ukishakuwa staa au msanii na watu wanakufuatilia basi pande zote mbili ni za kwako.

 

“Napenda sana Muziki zaidi komedi, ukitaka kuwaonesha watu kuwa unaweza kufanya vitu vingine tofauti na vile unavyofanya lazima uoneshe kwa juhudi kubwa, so mimi nikaweka juhudi zangu kuwa napenda muziki.

 

“Naweza muziki na nina thamini muziki na watu wakaelewa kuwa Whozu afanya komedi na pia anafanya muziki japo mwanzo hawakuamini amini,” amesema Whozu.

 

Leave A Reply