Whozu Tunda hawezi kunisaliti

BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa ameonekana hotelini akiwa na mwanaume mwingine mwenye asili ya Kinigeria, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Whozu amefunguka kuwa mpenzi wake, Tunda Sebastian hawezi kumsaliti hivyo habari hizo siyo za kweli.  Akizungumza na Showbiz, Whozu alisema watu wamekuwa wakizusha mengi kuhusiana na penzi lake na Tunda lakini hatetereki na mapenzi yao yapo palepale.

Whozu amezungumza mengi, ungana naye hapa chini; Showbiz: Inasemekana mmeachana na Tunda kwa sababu anatoka na mwanaume mwingine wa Nigeria, unazungu-mziaje?

Whozu: Mimi na Tunda hatujaachana, bado tupo poa na maisha yanaendelea kama kawaida. Watu wakae wakihaha na mitandao kusubiri Whozu aachane na Tunda.

Showbiz: Ukigundua kuwa Tunda anakusaliti, utafanyaje?

Whozu: Kwa kweli siku Tunda akinisaliti sitamsamehe, tutaachana tu kiroho safi bila shida yoyote.

Showbiz: Wewe na mpenzi wako Tunda mna malengo gani?

Whozu: Tuna malengo ya kufunga ndoa na ni lazima nimuoe Tunda kwa sababu mama yake ndiye mtu ambaye amekuwa akiniuliza hilo suala kila mara.

Showbiz: Zamani mlikuwa mnajiachia kwenye mahoteli mbalimbali mkila bata, kwa sasa hatuyaoni, imekuwaje?

Whozu: Kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira, kwa hiyo ni mambo tu yamebadilika, muda wa starehe upo tu kwa sasa ni kazi kwanza.

Showbiz: Watu wanasema Tunda amekupenda kwa sababu ya muziki, anajua kwamba ukifanya shoo mnapata fedha za kujiachia, hili likoje?

Whozu: Kupendwa na Tunda ni nyota na siyo muziki jamani, pia mimi nampenda sana Tunda kwa sababu ni mwanamke ambaye amekuwa akinishauri mambo makubwa sana kuhusu muziki ndiyo maana hata kwenye ngoma yangu ya Doko aliipenda na kuwa video queen.

Showbiz: Kuna habari kuwa kwa sasa umefilisika ndiyo maana wewe na Tunda hamli bata kama mwanzo, hili likoje?

Whozu: Siyo kwamba nimefilisika bali tumepumzika kwanza maana huwezi kujiachia kwenye starehe kila siku jamani.

Showbiz: Ngoma ya Huendi Mbinguni, ni wimbo ambao ulikutambulisha kwa kasi sana kutokana na video ilivyokuwa bora, unazungumziaje?

Whozu: Nilijisikia vizuri sana kwa sababu sikutegemea kabisa kama ingetokea hivyo pia nilimshukuru sana Mungu kwa maajabu aliyonifanyia, umenipa mafanikio makubwa hasa kujulikana.

Showbiz: Unazungumziaje shoo ya Diamond aliyoifanya hivi karibuni mkoani Kigoma ya kufikisha miaka 10 kwenye muziki wa Bongo Fleva?

Whozu: Amefanya jambo kubwa sana japo sikuwepo ila kwa kweli mtu akifanya vizuri mpe sifa zake, Diamond kwa kweli nampongeza kwa sababu amewapa nafasi wasanii kupafomu pia ni msanii ambaye ana roho nzuri.

Showbiz: Ni msanii gani ambaye alifanya vizuri mwaka 2019 ukasema kweli hili ni jembe la mwaka?

Whozu: Marioo ni msanii ambaye 2019 alifanya mambo makubwa ambayo mimi binafsi nilipenda kwa kweli, 2019 ulikuwa ni mwaka wake.

Showbiz: Kitu gani ambacho unakithamini na unachokipenda sana kwenye maisha yako?

Whozu: Napenda sana muziki hilo ni japo la kwanza, la pili napenda kufanya biashara maana nimetokea familia ya biashara.

Showbiz: Mashabiki wako watarajie nini kutoka kwako mwaka huu wa 2020?

Whozu: Huu ni mwaka ambao nimepanga kufanya mambo makubwa sana kwa hiyo mashabiki zangu wakae mkao wa kula pia waendelee kunisapoti na kunipa moyo pia kunikosoa pale ninapokosea na shukrani zangu za dhati ziende kwa Global Radio, Global TV na magazeti.

 

STORI KHADIJA BAKARI

Toa comment