The House of Favourite Newspapers

WIKI TATU TU YANGA MATAJIRI

MICHUANO ya Kombe la Kagame iliyopangwa kupigwa mwezi ujao Jijini Dar es Salaam huenda ikawa zali kwa Yanga ambayo kama ikicheza karata zake vizuri inaweza kufuta machungu ya msimu mzima wa Ligi Kuu Bara.

 

Zawadi za michuano hiyo ya wiki tatu ni kubwa kuliko zile za Ligi Kuu Bara ambayo inachezwa msimu mzima nyumbani na ugenini,ingawa kwa kutwaa ubingwa wa Kagame hawashiriki popote zaidi ya kutajirika. Bingwa wa Kagame anabeba Sh68milioni wakati bingwa wa Ligi Kuu Bara ambaye ni Simba anapewa Sh84milioni. Mshindi wa pili wa Kagame anachukua Sh45milioni na wa tatu Sh23milioni.

 

Zawadi hizo zinawaniwa na klabu mbalimbali za Ukanda wa Cecafa ambapo Tanzania itawakilishwa na Yanga, Simba na Azam ambao ni mabingwa watetezi. Kama Yanga na Simba mmoja wao akibeba kombe hilo, anapewa bonasi ya Sh250milioni na mdhamini wao SportPesa fedha ambayo tayari ipo kwenye maandishi.

 

Siyo hiyo tu, Yanga inasubiri bonasi yake ya Sh250milioni baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inayoendelea kwa sasa. Hivyo, kihesabu kama Yanga itapata zali hilo itakuwa imetengeneza Sh570 milioni ambayo huenda ikawapunguzia mzigo wa madeni wanayodaiwa na TFF na wachezaji wao.

 

Endapo Simba wakibeba na Kagame watakuwa na fungu kubwa zaidi msimu huu kiasi cha Sh494milioni. Simba inasubiri Sh184milioni kwa kutawazwa kuwa bingwa Tanzania kwani Sh84milioni ni zawadi ya bingwa VPL na Sh100milioni ni bonasi wanayopewa na SportPesa kwa mafanikio hayo.

Comments are closed.