The House of Favourite Newspapers

Mitandao yampa Samatta Uraia Congo, Wakati Marekani Ikimpa Uraia wa Tunisia

2
samatta (2)Mbwana Ally Samatta akikabidhiwa tuzo
samatta (3) Ulivyoandika mtandao wa Wikipedia kuhusu uraia wa Samatta kabla ya kurekebishasamatta (4)
Mtandao wa Wikipedia baada ya kurekebisha taarifa za uraia wa Samatta
Pamoja na umahiri wa mtandao wa Wikipedia lakini ajabu umeshindwa kujua uraia wa Mbwana Samatta anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo.
Badala yake umembandika uraia wa DR Congo na Tunisia ikiwa ni saa chache baada ya kubeba tuzo ya mwanasoka Afrika kwa wanaocheza barani Afrika.
Mtandao huo maarufu duniani ulionyesha Samatta ni raia wa DR Congo. Lakini baada ya saa kadhaa ulibadili na kuweka taarifa mpya inayoonyesha kuwa uraia wake ni Tanzania ikiwa ni sehemu ya kurekebisha kosa hilo.samatta (1)Ilivyoandika NBC ya Marekani
Kwa upande mwingine, mtandao wa runinga maarufu ya NBC ya Marekani, wao wamembandika Samatta uraia wa Marekani.
Kupitia mtandao wao wa www.nbcsports.com wameandika Samatta ni mchezaji bora Afrika kwa wanaotokea ndani ya Afrika akiwa anatokea nchini Tunisia!
Kabla ya hapo, mtandao mwingine wa wikipidia nao ulimbandika Samatta uraia wa RD Congo.
Mtandao huo maarufu duniani ulionyesha Samatta ni raia wa DR Congo. Lakini baada ya saa kadhaa ulibadili na kuweka taarifa mpya inayoonyesha kuwa uraia wake ni Tanzania ikiwa ni sehemu ya kurekebisha kosa hilo.
2 Comments
  1. Alfred Boota says

    Hongera zako Samatta,

  2. Donnie says

    Swadaktah!

Leave A Reply