The House of Favourite Newspapers

Willian, Ozil wapasua usajili wa PSG

WAKATI dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Paris Saint-Germain ilikuwa ikipambana kuhakikisha inamsajili winga wa Chelsea, Willian.

 

Mabingwa hao wa Ufaransa walikuwa wakihaha kuhakikisha wanafanikisha dili hilo kwa pauni milioni 40 ili kuziba nafasi ya Neymar ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10 kutokana na kuwa majeruhi.

 

Awali, PSG ilikuwa ikihitaji kumsajili staa wa Arsenal, Mezut Ozil kwa mkopo lakini ikaelezwa kuwa hadi jana jioni mchezaji huyo alikataa dili hilo la mkopo.

 

Kuwa nje kwa Neymar kumeipa pigo PSG ambayo pia itamkosa katika michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester United.

Hivyo hadi tunaingia mitamboni bado mambo yalikuwa hayajaeleweka na lolote linaweza kutokea kuhusu Willian ambaye ni Mbrazili mwenye umri wa miaka 18 ambaye mkataba wake ndani ya Chelsea ulikuwa umesalia miezi 18.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.