The House of Favourite Newspapers

Winga la Kazi Nakuja Yanga… Azungumza na Championi Jumatano Akiwa Uganda

0
Winga wa pembeni wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello.

 

WINGA wa pembeni wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello ameweka wazi kuwa tayari kujiunga na Yanga endapo viongozi wa timu hiyo watakuwa tayari kuhitaji saini yake na kufanya mazungumzo kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Okello mwenye umri wa miaka 22 ni moja kati ya wachezaji bora chipukizi kutoka nchini Uganda mwenye uwezo mkubwa wa kutumia guu la kushoto ambaye amewahi kutamba na kikosi cha timu ya vijana cha Uganda chini ya umri wa miaka 17 akiwa katika kizazi kimoja na Kelvin John anayekipiga KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

Kwa sasa winga huyo anakipiga kwa mkopo katika klabu ya KCCA ya Uganda akitokea Klabu ya Paradou AC inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria.

Akizungumza na Championi Jumatano moja kwa moja kutoka nchini Uganda, Okello aliweka wazi kuwa tayari kujiunga na klabu ya Yanga endapo watahitaji huduma yake na watafuata taratibu zote za usajili huku akiweka wazi kuwa Yanga ni moja kati ya timu kubwa na bora kwa sasa Afrika Mashariki jambo ambalo wachezaji wengi hutamani kuchezea timu hiyo.

“Yanga ni moja kati ya timu kubwa na nzuri kwa sasa katika ukanda wetu hivyo ni ndoto kwa wachezaji wengi kucheza, kwa upande wangu siwezi kusema kuwa kama Yanga watanihitaji basi nitakataa sio kweli, kama Yanga wao watakuwa wananihitaji basi wanatakiwa kufuata taratibu na kama watakamilisha mimi nitakuwa tayari kujiunga nao.

“Kuhusu mimi kuwa kwenye mazungumzao na viongozi wa Yanga ni ngumu kulizungumza kwa sasa kwani ni nje ya utaratibu wa maadili yangu nikiwa kama mchezaji nikiwa na mkataba na timu nyingine, nadhani hilo lipo wazi,” alisema winga huyo.

Stori: Marco Mzumbe, Championi Jumatano

KOMBE la DUNIA: MWAMUZI wa KIKE wa AFRIKA ATIKISA DUNIA HUKO QATAR…

Leave A Reply