The House of Favourite Newspapers

Wizara ya Afya Yawasisitiza Mitishamba Kupambana na Changamoto za Upumuaji

0

 

Wakati Watanzania wengi wakipambana na maradhi mbalimbali yanayosababisha changamoto za upumuaji, ikiwemo nimonia na Corona, wizara ya afya imeendelea kuwasisitiza wananchi kutumia dawa za mitishamba kupambana na magonjwa mbalimbali.

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima na naibu wake, Dk. Godwin Mollel wameyasema hayo kwa nyakati tofauti walipotembelea banda la maonesho la Kampuni ya Natural Therapy LTD jijini Dodoma na kujionea dawa mbalimbali zinazotengenezwa kwa mitishamba na virutubisho ili kutibu magonjwa mbalimbali.

 

Baada ya kufika kwenye banda hilo, walikutana na Mkurugenzi wa Natural Therapy LTD, Tabibu Riziki ambaye aliwafafanulia kuhusu dawa mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni hiyo, ikiwemo Imunno Booster yenye uwezo mkubwa wa kupandisha kinga ya mwili na kupambana na maradhi mbalimbali ikiwemo changamoto za upumuaji.

 

Kwa upande wake, Waziri Gwajima alimpongeza Tabibu Riziki kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuelekeza nguvu zaidi katika kugundua dawa za mitishamba zenye uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mbalimbali, ikiwemo changamoto za upumuaji na Corona.

 

Pia alitoa wito kwa wataalamu wa tiba asili kuongeza juhudi za kugundua dawa za asili za kupambana na maradhi mbalimbali huku pia akiwataka Watanzania watumie dawa za asili sambamba na kufuata maelekezo mengine ya wataalamu wa afya katika kujilinda na maradhi mbalimbali, ikiwemo ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Gwajima naye alitoa pongezi kwa wataalamu wa tiba asili wanaoendelea kugundua dawa mbalimbali za mitishamba na kuwataka kuendelea kuumiza vichwa kutafuta dawa zitakazomaliza kabisa changamoto za upumuaji na magonjwa mengine kama Corona kwa Watanzania.

 

Kwa upande wake, Tabibu Riziki alionesha kufurahishwa na jinsi viongozi hao wa juu katika wizara ya afya wanavyowaunga mkono wataalamu wa tiba asili katika mapambano dhidi ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua Watanzania.

“Tunazo dawa nyingi hapa ikiwemo hii ya Immuno Booster ambayo inatengenezwa kwa virutubisho asilia vyenye uwezo wa kuongeza madini ya Calcium na Vitamini C. Pia virutubisho hivi husaidia kukinga na kuulinda mwili dhidi ya saratani, maambukizi ya virusi ikiwemo Flu, SARS, Covid 19 na kujikinga na uvimbe na miwasho mbalimbali mwilini.

 

“Kama hiyo haitoshi, Immuno Booster inasaidia kuongeza kinga kwa watu wenye aleji mbalimbali za mafua, ngozi na kubanwa na kifua na hata watu wenye changamoto za upumuaji Immuno Booster huwasaidia sana,” anaeleza Tabibu Riziki.

 

“Ofisi zetu zipo Ubungo Plaza, ‘ground floor’ kwa jijini Dar es Salaam lakini dawa zetu zinapatikana nchi nzima kupitia kwa mawakala wetu. Unaweza kuwasiliana nami kwa namba za simu 0744111115 au 0753185 592,” anahitimisha Tabibu Riziki.

 

 

Leave A Reply