Wizkid Adondosha Wino Na RCA Records/ Sony Music International Na Kuachia Wimbo Mpya; ‘Sweet Love’ – (Video)

Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid anazidi kupasua anga kulitafuta soko la muziki duniani.

Mmiliki wa Starboy Entertainment Worldwide Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kama Wizkid amesign mkataba mnono wa kurekodi album na label kubwa wa muziki Marekani RCA Records/ Sony Music International akijiunga rasmi na ukoo mkubwa wa wasanii wa kimataifa kutoka kwenye label hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya RCA Records, Chairman na CEO, Peter Edge alisema:

Tunafurahi kumkaribisha Wizkid kwenye familia ya RCA Records. Amekuwa nyota kubwa sana wa muziki wa Africa na anakuja kuibadilisha historia kwa kuupeleka muziki wa Africa duniani. Tunafuraha kubwa sana kuwa nae hapa RCA tukiwa tumejawa na uchu wa safari iliyopo mbele yetu.

Naye Wizkid ambaye baada ya taarifa hiyo kuachiwa, alidondosha wimbo mpya Sweet Love’ na kuiambia Billboard:

Ni vigumu kwa mimi kueleza nafanyaje fanyaje, maana nacheza tu na midundo ya Afro-Beats, Raggae, Hip-Hop, Dancehall na nyinginezo. Kitu cha muhimu kwangu ni muziki uwe real, wa kipekee na usiopoteze ladha. Sitaki kujifunga au kuwekwa kwenye aina moja ya muziki.

RCA Records ni nyumbani kwa wasanii wa kubwa wa muziki duniani kama Alicia Keys, Chris Brown, Britney Spears, Justin Timberlake, R Kelly, Shakira, TPain, Tinashe, pamoja na Davido kutoka Nigeria na wengine wengi, na sasa sehemu hiyo ni makazi mapya ya mkali huyo kutoka Africa.

Itazame ngoma mpya wa Wizkid ‘Sweet Love’ hapa chini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.Tecno


Toa comment