The House of Favourite Newspapers

WIZKID ALIPWA BIL. 1 KUFANYA SHOO HARUSINI

Wizkid

STAA wa muziki kutoka nchini Nigeria amepata shavu la kupafomu kwenye harusi ya kifalme nchini India kwa malipo ya shilingi bilioni 1.

 

Kwa mujibu wa chanzo kinasema staa huyo ‘alipafomu laivu’ na bendi yake katika shoo hiyo iliyofanyika katika Jumba la Umaid Bhawan huko India, sehemu yenye makazi binafsi ya matajiri wakubwa duniani, kati ya nyimbo ambazo aliziimba katika sherehe hiyo ni Soco na Fake Love.

Shavu hilo linamfanya, Wizkid kuingia katika listi ya wasanii wanaolipwa pesa kiwango cha juu zaidi kwenye shoo za kimaifa mbalimbali.

Comments are closed.