The House of Favourite Newspapers

Wizkid Amburuza Diamond Tuzo za MTVEMA

0

MSANII wa kimataifa kutoka pande za Nigeria, Wiz Kida ameshinda Kipengele cha BEST AFRICAN ACT (Msanii Bora wa Afrika) kwenye Tuzo za MTV EMA mwaka 2021.

Tuzo hizo za MtvEma zinaendelea kutolewa usiku jana katika Ukumbi wa Budapest Sportarena nchini Hungary.

Katika kipengele hicho cha Best African Act @wizkidayo alikua akichuana na @diamondplatnumz, @amaarae, @temsbaby, @focalistic ambapo wote amewafunika.

Ikumbukwe kwamba, waka 2016 katika kipengele hicho hicho alitangazwa Wizkid kuwa mshindi na kupewa tuzo hiyo, lakini baadae ilionekana Alikiba ndiye alikuwa mshindi halali kutokana na kura zilivyokuwa zikionyesha, hivyo Wizkid akanyang’anywa tuzo hiyo na kupewa Alikiba.

Leave A Reply