Wizkid atua Dar, tayari kwa shoo yake Leaders leo

WIZKID IN DAR (2)

Wizkid baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) usiku huu.

WIZKID IN DAR (3)

Wizkid akisindikizwa na walinzi mara baada ya kuwasili Dar usiku huu.

WIZKID IN DAR (1)

WIZKID IN DAR (8)

Warembo wakisubiri kumpokea Wizkid.

4

WIZKID IN DAR (5)

Wizkid akiongea na wanahabari waliofika kumpokea usiku huu.

WIZKID IN DAR (6)

Wizkid akielekea kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea hotelini.

WIZKID IN DAR (7)
Gari lililombeba Wizkid.

MWANAMUZIKI mahiri kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kama Wizkid ametua nchini usiku huu tayari kwa onyesho lake litakalofanyika hapo baadaye kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Staa huyo amewasili nchini majira ya saa 7 na kuwasalimia mashabiki wake waliofika uwanjani hapo kumpokea huku akitoa maneno ya utani kuwa amekuja kuwaona warembo wa Tanzania.

Wizkid ambaye anafanya vizuri kwa wimbo wake wa Ojuelegba atafanya onyesho kubwa la kihistoria Afrika Mashariki, chini ya usimamizi wa Kampuni King Solomoni Entertainment.

Msanii huyo anatarajia kuzikonga nyoyo za mashabiki kwa vibao vyake vikali vikiwemo; Show You the Money, Caro, In My Bed, On Top Your Matter, Holla at Your Boy, Jaiye Jaiye, Expensive Shit, Love My Baby, Omalicha, Celebrate na vinginevyo kibao.

(HABARI/PICHA: Clarence Mulisa na Musa Mateja / GPL)


Loading...

Toa comment