The House of Favourite Newspapers

Wizkid Awakubali Diamond, Kiba

0

Wizkid.

Mkali wa muziki toka Naija anayetamba kwa kibao chake cha Ojuelegba, Wizkid ameonesha kuwakubali wanamuziki kutoka Tanzania ambao ni Diamond Platnumz na Ali Kiba jambo lililoonesha jinsi muziki wa Bongo Fleva ulivyofika mbali.

Diamond Platnumz.

Wizkid alisema hayo katika shoo iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar wikiendi iliyopita ambapo mbali na kuwakubali wasanii hao alionesha mapenzi yake ya dhati kwa mashabiki Bongo kwa mapokezi aliyoyapata kabla ya kuangusha shoo ya nguvu na kupiga vibao vyake kama Caro, Show You The Money, On Top Of Your Matter na Ojuelegba.

 Ali Kiba.

Msanii huyo alipanda jukwaani akitanguliwa na msanii Christian Bella aliyepanda na bendi yake ya Malaika, Fid Q na Diamond Platnumz

Leave A Reply