The House of Favourite Newspapers

Wizkid kupamba jarida kubwa duniani la Vogue

0

00-holding-wizkidStaa wa Ngoma ya Ojuelegba, Wizkid.

STAA wa Ngoma ya Ojuelegba, Wizkid kwa mara ya kwanza amepata shavu la kimataifa na anatarajiwa kulipamba jarida kubwa la habari za mastaa na wanamitindo duniani lijulikanalo kama Vogue.

Wizkid mwenye miaka 25 ambaye pia ni balozi wa kinywaji cha Pepsi nchini Nigeria, katika jarida hilo alifanyiwa mahojiano juu ya kazi zake na maisha yake kwa ujumla.

Toleo la mwisho la jarida hilo lilimtoa staa wa muziki kutoka Uingereza Adele.

adele-vogue-cover-march-2016

Hii inamuweka Wizkid kuwa miongoni mwa mastaa waliowahi kutolewa na jarida hilo ambapo kabla yake walishawahi kutolewa kina Kylie Jenner, Kim Kardashian, Kanye West, Beyonce, David Beckham na wengine wengi.

(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

 

 

Leave A Reply