#GlobalCelebrityUpdates: Wizkid Na Drake Kufanya Collabo Nyingine?

Siku hizi ukitaka kujua msanii gani anafanya nini, wapi, lini na nani isogelee tu Instagram au Twitter, huko utapata majibu ya maswali yako yote.

Baada ya kufanya vizuri na wimbo wao wa ‘One Dance’, kuna uwezekano wa Wizkid na Drake kushirikiana tena kwenye kazi nyingine. Hivi karibuni Wizkid alikuwa location akishoot video ya wimbo wake mpya ‘Come Closer’ kazi inayosemekana imeshirikisha Drake (hapo awali kabla ya kuvuja wimbo huu ulikuwa jina la ‘Hush Up The Silence’), na kwa picha chache alizozipost za BTS inaonekana kuna uwezekano mkubwa pengine Drake kuwepo kwenye wimbo huo.

Februari 2 2017 moja ya akaunti za Twitter zinazohusika na kuposti updates mbalimbali za drake @The6Track, walipost tweet kutangaza mabadiliko ya la wimbo huo wa Wizkid:

Tarehe ya lini video hiyo itaachiwa haijulikani bado na Wizkid hajaweka wazi kama Drake atakuepo kwenye video hiyo na wala Drake hajazungumza chochote kuhusu video hiyo mpaka sasa.

Kwa sasa Wizkid yupo studio anakamilisha International album yake iliyopewa jina ‘Sounds From The Other Side’ project ambayo kwa mujibu wa staa huyo ni project kali aliyoifanya mpaka sasa.

Hizi ni baadhi ya picha za Behind The Scenes za video mpya ya Wzikid.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.
Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.Toa comment