Wizkid wa Bongo Amfungukia Amber Lulu
MKALI wa Ngoma ya Ibe na Sawala, Gib Carter ‘Wizkid wa Bongo’, amefungukia muuza nyago wa kwenye video za Kibongo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Amber Lulu kuwa licha ya kusemwa hovyo mitandaoni yeye anamchukulia kama msanii anayejitambua kimataifa.
Akichonga na Star Showbiz, Gib Carter anayebamba na Ngoma ya Namba alisema, mara nyingi Amber Lulu amekuwa akitisa mitandaoni baada ya kufanya vitu ambavyo kwake anaona kama anaenda na wakati.
“Mbona vitu anavyofanya Amber havina tofauti kabisa na anavyofifanya Kim Kardashian, Blac Chyna au Amber Rose. Nawashangaa sana akijiachia kidogo au kuwa close kimahaba na mtu basi imekuwa shida,” alisema Gib Carter anayefananishwa hadi uimbaji na staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid.
Comments are closed.