The House of Favourite Newspapers

Wolper Adai Amependa Alichofanya Kizz Daniel, Awaelezea Wanawake Wenzake

0
Jackline Wolper

MSANII maarufu wa Bogo Movies, Jacqueline Wolper ‘Mama K’ ameshindwa kuzuia hisia zake na kuibuka kuzungumzia sakata la supastaa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Oluwatobiloba Daniel Anidugbe maarufu kama Kizz Daniel kukacha shoo ya Summer Amplified aliyotakiwa kufanya usiku wa kuamkia jana Agosti 8, 2022 jijini Dar.

 

Wolper ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha hit-maker huyo wa ngoma ya Buga inayofanya vizuri kupitia mitandao ya kijamii kuingia mitini huku mashabiki wakipiga miayo ya kumsubiri ukumbini.

 

Kupitia Instastory yake, Wolper ameweka picha ya Kizz Daniel na kuandika; “Nafurahi ulichofanya jana maana hata ndoa zilitaka kuvunjika watu wamerudi asubuhi bwana Buga lakini bila kusahau wadada wamekopa na kukopwa kwa ajili ya nguo mpya na mawigi mapya, watu walijipanga kusema ukweli nimependaa hahahaha nakojoa jamani,” ameandika Wolper.

Kizz Daniel

Inaelezwa kuwa, Kizz aligoma kufanya shoo hiyo kwa sababu ya kutokuwepo nguo zake ambazo kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ni kuwa alisahau nguo hizo nchini Kenya.

 

Pia, inadaiwa kuwa hata cheni yake aliyopanga kuivaa aliisahau Nigeria hivyo akagoma kupanda jukwaani kutokana na kukoseakana kwa vitu vyake hivyo muhimu.

Licha Kizz kutua kwenye ardhi ya Tanzania staa huyo hakufanikiwa kufanya shoo hiyo jambo lililosababisha kukamatwa na kupelekwa katika kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alishikiliwa kwa saa kadhaa kabla ya Harmonize kumwekea dhamana na kumtoa lupango.

 

Licha ya Kizz kutotokea jukwaani mastaa wengine kutokea nchini Tanzania kama Marioo, Saraphina, Mabantu na Young Lunya walifanikiwa kutoa burudani kwenye shoo hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa #WareHouse zamani Nextdoor.

Leave A Reply