The House of Favourite Newspapers

WOLPER AFUNGUKIA ‘KUTOKA’ NA LORD EYES

Jacquline Wolper

STAA mkali wa filamu Bongo, Jacquline Wolper amefungia madai ya kutoka kimapenzi na Rapa Waziri Makuto ‘Lord Eyes’ kwa kusema kuwa hayana ukweli.  

 

Akizungumza na Ijumaa, Wolper alisema yeye ameona kwenye mitandao taarifa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Lord lakini pia hata siku ikitokea ikawa hivyo sio mbaya kwani sio mwanaume mbaya kwake na pia anavutiwa na jinsi alivyo.

 

“Unajua hata mimi ambaye naambiwa natoka naye nimeona kwenye mitandao tu lakini pia siku ikitokea, freshi tu.

 

Sio mwanaume mbaya maana ana sifa zote za mwanaume ninayempenda au wamesema hivyo kwa sababu niliimba wimbo wake nikauposti mtandaoni ndio tatizo basi ngoja tuone itakavyokuwa maana Wabongo wape picha tu maneno wataweka mwenyewe.”

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.