Wolper Ahamia Uswazi, Ataja Sababu

NANI amekwambia mastaa hawawezi kupiga mzigo wakiwa uswahilini ‘uswazi’ na mambo yakaenda? Basi huyu hapa binti wa Massawe, Jacqueline Wolper kwa sasa anapiga kazi maeneo ya uswazi huko Tandika na mambo yanaenda shwari.

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Wolper alisema kuwa kufanya kazi ni popote lakini Tandika nako kuna wateja wake tofauti na Kinondoni alipokuwa, ndiyo maana akaamua kuingia mzimamzima uswazi na kushusha mastaili yake ya kishuani.

“Unajua sisi wengi tumejisahau na kuamini wateja wapo maeneo ya Kinondoni, Sinza na sehemu nyingine na wakati huko uswazi kuna watu wanahitaji huduma zangu lakini hawazipati kwa wakati,” alisema Wolper.

 

IMELDA MTEMA, DAR


Loading...

Toa comment