Wolper Alivyokata Keki na Mastaa The Life Club, Dar

Esma Platnumz, dada wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz,  akilishwa keki na mwigizaji Jacqueline Wolper, usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa The Life Club ulioko Mwenge jijini Dar es Salaam.

Usiku wa Desemba 7, 2018, mwigizaji wa Bongo Movie na mwanamitindio, Jaqueline Wolper, alisherehekea siku yake ya kuzaliwa katika ukumbi wa Life Club Mwenge ambapo wapenzi Sarah na Harmonize walinogesha sherehe.

Mastaa waliofika kusherekea na Wolper siku yake ya kuzaliwa ni Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’, Lavalava, Esma Platnumz, Video vixen Nai, Amber Lulu, Gigy Money na wengine kibao.

Meneja wa Burudani wa The Life Club, Hemed Kavu ‘HK’ akimwita staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper kupanda stejini.

…Wolper akiongea na mashabiki (hawapo pichani) baada ya kupanda stejini.

Staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ akilishwa keki na Wolper.

Video vixen Nai ambaye ni mpenzi wa Moni Centrozoni akilishwa keki.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Toa comment