The House of Favourite Newspapers

Wolper Amtuliza Sarah kwa Harmonize!

0

DAR: Kiroho safi! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, amemtuliza mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Sarah Michelotti kwa kumwambia asiwe na shaka, wao mapenzi yaliisha zamani, sasa hivi wamebaki kuwa washkaji tu!

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA hivi karibuni kwenye maonesho ya Sabasaba, Wolper alisema, kitendo cha Harmonize au Harmo kutembelea kwenye banda lake lililokuwa katika viwanja hivyo kumuungisha, ni jambo jema na watu watambue wao siyo maadui kama walivyokuwa wakifikiria hadi kumpa presha Sarah.

“Naamini kabisa watu wengi walijua wazi mimi na Harmo tuna matatizo au tuna uadui, lakini ukweli ni kwamba, hatuna matatizo, ni watu tunaoheshimiana kwa sasa na anasapoti harakati zangu na mimi nasapoti muziki wake,” alisema Wolper.

Harmo aliongeza kuwa, hata Sarah alikuwa akipata wivu kutokana na maneno ya watu ambao kila kukicha wanapenda kuona watu wako na tofauti, hivyo wajue kuwa yeye na Harmo ni watu wanaoheshimiana.

“Watu ndiyo walikuwa wanachochea ugomvi hadi kumpa Sarah wasiwasi, lakini ukweli ni kwamba, tuko vizuri sana na hakuna tatizo lolote kati yangu na Raj (Harmo) na wala hatuna uadui kama walivyoona, kila mmoja anasapoti anachofanya mwenzake,” alisema Wolper ambaye sasa hivi ni muuza vitenge maarufu.

Wolper na Harmo, waliwahi kuwa wapenzi kabla Harmo hajahamishia majeshi kwa Sarah, raia wa Italia na kufunga naye ndoa ya kimila.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa

Leave A Reply