The House of Favourite Newspapers

Magufuli Ampa Maagizo Mazito Mwakyembe – Video

0

RAIS wa Tanzania John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe kuhamishwa kwa chombo kinachosimamia sanaa Tanzania (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

amesema hayo leo Ikulu Chamwino katika ghafla ya chakula cha mchana alipokula na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya CCM kufuatia mwaliko wake.

 

Amesema kuwa waziri mwenye dhamana kabla ya kwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimboni kwake anapaswa kupeleka barua ili aweze kuisaini.

 

“Niwapongeze wasanii mmeitangaza Tanzania kwa maslahi mapana, Serikali iko pamoja nanyi kuhakikisha inatetea maslahi yenu, najua mmeteseka sana nahitaji mtoke huko COSOTA na kuingia kwenye Wizara ya Habari ili kazi zenu zionekane na mfaidike,” amesema Magufuli.

 

Amesema COSOTA ilishindwa kuwasimamia vizuri wasanii na kazi zao jambo ambalo limesababisha wasanii kuteseka kwa muda mrefu kwani wapo waliotumia kazi zao kwa manufaa binafsi. Amesema kuwa kuitoa huko itasaidia kwa kiasi kikubwa wasanii kuepukana na changamoto wanazokumbana nazo.

 

“Serikali inatambua kazi wanayofanya wasanii kwa kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi hivyo niwatake kuendelea na ushirikiano wenu ili kulisongesha taifa mbele.” alisema Magufuli.

Leave A Reply