The House of Favourite Newspapers

Wolper Atoa Ahadi kwa Wema Sepetu Akipata Mimba Kumfungia Ndani… Video

0

 

 

Jacqueline Wolper.

Muigizaji mkongwe nchini Tanzania, Jacqueline Wolper amemwandikia muigizaji mwenzake, Wema Sepetu akimwambia kwamba siku atapata ujauzito, atakuwa mtu wa kwanza kujitolea na kumfungia ndani akimhudumia kwa kila kitu ilimradi asiteseke kipindi chote cha ujauzito.

Wema Sepetu alikuwa ameposti angalizo akisema kwamba hakuwa na ujauzito, bali ni kipindi tu watu waliona mahali akiigiza kuwa ni mjamzito.

Wema Sepetu.

Sepetu ambaye amekuwa akionesha nia na tamaa kubwa ya kupata angalau mtoto wake naye siku moja alisema kwamba hakuwa na ujauzito na ikitokea siku moja atapata mimba wala hatamueleza mtu yeyote kwani itakuwa siri yake. “Angalizo..!!! Kile ni kipindi…bado mimi sina ujauzito…!!! Na hata kama nikishika mnahisi nitasema kweli…? Yaani ndo ile Mungu kasema, “Sasa acha nikubariki tumbo lako Wema”, halafu paap “MIMBA”…Sisemi Ng’o…!!! Ila naitamani jamani…Tuseme Inshallah… “ Wema Sepetu aliweka wazi.

Leave A Reply